Yanga yaidhibiti Simba kila kona ya Dunia hii - The Choice

Yanga yaidhibiti Simba kila kona ya Dunia hii

0

 

Mashabiki wa Simba na Yanga

WASIMAMIZI wa Soka la Afrika (CAF) wametoa tamko zuri kwa timu za Bara zima ambalo huenda likawa shangwe kubwa kwa timu za Bongo kuanzia mwakani. Lakini furaha hiyo haitawahusu Simba hata kwa mbeleko ya aina gani kutokana na mwenendo mbovu wa Yanga na Azam kwenye michuano ya kimataifa tangu 2011

CAF imetangaza kwamba kuanzia mwakani hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa na timu 16 badala ya nane za awali. Tamko hilo litakuwa neema kwa nchi kadhaa za Afrika ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kwenye michuano yote miwili kwani zitaongezewa idadi ya timu shiriki.

Simba ikimaliza ya pili kwenye Ligi msimu huu itakuwepo? Sahau hilo. Taarifa mbaya ni kwamba Tanzania si mojawapo ya nchi hizo zinazoweza kufikiria kwenye ofa hiyo.

Timu zinaongezwaje 2017?

CAF inaangalia mwenendo wa klabu za nchi husika kwenye michuano yote miwili kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015. Ambapo ili nchi ipate ofa lazima iwe iliingiza timu mara zote kwenye makundi ya michuano yote na ziwe zilifanya vizuri kwavile kila nafasi kwenye kundi ina pointi ambazo timu husika inapewa.

Kigezo hicho kimeitoa Simba moja kwa moja kwani Azam na Yanga ambazo zimekuwa zikibadilishana ndani ya miaka hiyo zimefanya vibaya na hazijaingia makundi. Simba ilishiriki Shirikisho mwaka 2012 na mabingwa 2013 na mara zote ikachemka mapema kama Yanga na Azam.

Tamko la CAF

Rais wa CAF, Issa Hayatou ametoa ufafanuzi huo juzi Jumatano kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho hilo uliofanyika Mexico.

Kwa mujibu wa Hayatou michuano ikitoka kwenye hatua ya mtoano itaingia kwenye raundi ya kwanza ambapo ikishinda katika hatua hiyo ndiyo moja kwa moja kwenye makundi.

Kwa utaratibu wa awali klabu ikitoka kwenye raundi ya kwanza inaingia raundi ya pili kisha ikifuzu inakwenda makundi

Facebook Comments
Share.

About Author