Home News ZIWA MANYARA HATARINI KUTOWEKA SERIKALI YAASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI MADHUBUTI

ZIWA MANYARA HATARINI KUTOWEKA SERIKALI YAASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI MADHUBUTI

811
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba (katika) akiongea na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wa
Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Murad Sadick mara baada ya kutembelea Ziwa
Manyara kuona hali halisi ya Ziwa hilo kwa sasa ambalo liko hatarini kutoweka
kutokana na ongezekeo la shughuli za kibadamu pembezoni mwa ziwa hilo zisizo
endelevu. Wengine pichani, ni sehemu wa waheshimiwa wabunge, wajumbe wa Kamati
hiyo.

Ziwa Manyara linavyo onekana kwa sasa, kina cha maji kimeshuka sana kutokana na
kujaa tope. Kamati ya Bunge imeshauri Serikali kuchukua hatua za haraka kunusuru
kutoweka kwa ziwa hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge wa Viwanda, Biashara
na Mazingira mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kutembelea Ziwa Manyara
kuona changamoto za uharibifu wa mazingira utokanao na shughuli zisizo endelevu za
kibinadamu ikiwemo kilimo katika vyanzo vya maji.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lulu Mussa
Manyara
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeshauri Serikali kuandaa
mpango Mkakati wa haraka wa kunusuru Ziwa Manyara ambalo liko hatarini kutoweka kutokana
shughuli za kibadamu. Akizungungumza kwa niaba ya Kamati yake Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mheshimiwa Murad Sadick amesema ni wakati muafaka sasa jambo hili kupewe
kipaumbele ili kunusuru hali ya sasa inayotishia uhai wa ziwa hilo.
Wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Manyara, Kamati hiyo imetembelea Ziwa Manyara na
kujionea kupungua kwa kina cha maji kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli za kibinadamu
ikiwa ni pamoja na kilimo kisicho endelevu hususan katika vyanzo vya maji kinachopelekea
ziwa hilo kujaa tope pamoja na ongezeko la mimea vamizi.
“Sote tumejionea hali halisi, hali ni mbaya, mimi na Kamati yangu tunawajibu wa kuishauri
Serikali, hatua za haraka na za maksudi kunusuru hali hii, hata kwa maziwa mengine pia kama
Ziwa Jipe na Ziwa Chala. Endapo hatua za haraka hazitachukuliwa ndani ya miaka kumi ijayo
Ziwa hili litatoweka. Ikumbukwe kuwa ziwa hili ni chanzo kikubwa cha kukuza pato la Taifa
kupitia Utalii hapa nchini” Alisisitiza Mhe. Sadick.
Akiwasilisha hatua za zilizochukukuliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
kuhusu kunusuru ziwa hilo Naibu Mkurugenzi Bw. William Mwakilime amesema kuwa Ofisi
yake imechukua hatua za makusudi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa Umma juu ya namna
bora ya kuwa na kilimo endelevu kinachozingatia matumizi bora ya ardhi na kujenga mabwawa
maalumu kwa ajili ya kuchuja maji.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mheshimiwa January
Makamba alieambatana na Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge katika ziara hiyo, amesema
Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha andiko jumuishi litakalogusa sekta zote kwa
kuwa ni suala mtambuka na kuahidi kuwa Serikali inalipa uzito jambo hilo kwa mustakabali wa
nchi na ustawi wa wananchi wake.
Katika hatua nyingine Kamati imeipongeza Serikali kwa kupokea ushauri wa Kamati hiyo ya
kuunda kikosi kazi cha kupambana na mimea vamizi ambayo imekuwa ikiathiri maeneo mengi
hapa nchini ikiwa ni pamoja na maeneo ya Hifadhi. Waziri Makamba ameainisha kuwa Kikosi
kazi hicho kilichoundwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais kimekamilisha kazi na taarifa yake
iko katika hatua za maamuzi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iko katika ziara ya kikazi
Mkoani Arusha pia itatembelea miradi ya uchimbaji wa visima Bagamoyo Mkoa wa Pwani,

ikiwa ni miongoni mwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Mkataba
wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.